Pages

Translate

Sunday, 21 July 2013

MWANAMKE ALIYESINGIZIA KABAKWA AGEUZIWA KIBAO NA KUFUNGWA MIEZI 16 JELA



Utambulisho wa mwanamke raia wa Norway ambaye amehukumiwa kifungo cha miezi 16 jela kwa kutembea nje ya ndoa baada ya kuwa ameripoti kubakwa mjini Dubai, umewekwa hadharani kwa mara ya kwanza jana.

Akitabasamu kwa furaha kwenye kamera, Marte Deborah Dalelv alionekana kama hana anachojali katika hii dunia.

Lakini mwanamke huyo mwenye miaka 24 alikuwa amebakwa akiwa kwenye safari ya kibiashara katika Umoja wa Falme za Kiarabu na alihukumiwa kwenda jela kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa baada ya kuwa ameripoti tukio hilo polisi.

Marte aliripoti shambulio hilo la ubakaji Machi mwaka huu, baada ya kuwa amekaa siku kadhaa rumande kabla ya kuruhusiwa kutumia simu.

Kwa msaada wa wanafamilia, ubalozi wa Norway ulifanikiwa kuafikiana kumwachia na amekuwa akiishi chini ya ulinzi wa Kanisa la Norwegian Sailor hadi wakati wa hukumu yake wiki hii.

"Nimepokea hukumu kali zaidi kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa, hukumu kali zaidi kwa kunywa pombe na zaidi ya yote nilipatikana na hatia ya kusema uongo," alieleza.

"Ni hatua ya kushangaza yuko ndani," alisema Gisle Meling, mchungaji katika Kanisa la Norwegian Sailor.

"Tumeshangazwa mno na tulitumaini ingekwenda kivingine, lakini tunaishi kwenye nchi ambayo ina mfumo wa sheria ambao unatoa maamuzi yake kwa msaada wa Sharia."

Marte alihukumiwa mwaka mmoja na miezi minne jela lakini kutokana na Norway kutokuwa na mkataba na Dubai wa kurejesha mkosaji ahukumiwe nchi alikotoka, hatima yake haijajulikana.

Habari ya mwanamke huyo kijana wa Norway sio ya kipekee.

Mapema mwaka huu, raia wa Australia Alicia Gali mwenye miaka 27, alizungumza jinsi alivyotupwa jela mjini Dubai kwa miezi minane baada ya kuripoti kubakwa.

Alicia alikuwa akifanya kazi kwenye eneo lenye mahoteli la Starwood ndipo kinywaji chake kilipotobolewa na kitu chenye ncha kali kwenye baa ya wafanyakazi.

Alizinduka na kugundua kwamba wenzake watatu walikuwa wamembaka, lakini alipokwenda hospitali kwa msaada, walimgeuka kwa polisi na akashitakiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.

Chini ya sheria za Umoja wa Falme za Kiarabu, wabakaji wanaweza tu kutiwa hatiani kama endapo mhusika anakiri mwenyewe au kama wanaume wanne wa Kiislamu watu wazima wameshuhudia uhalifu huo.

Chini ya sheria zinazofuata hukumu za Kiislamu za Sharia, ngono kabla ya ndoa imekatazwa kabisa na wapenzi ambao hawajaoana wakishikana mikono hadharani wanaweza kufungwa jela.

Wageni wanaofungwa mjini Dubai hurejeshwa mara moja makwao wanapomaliza adhabu zao.

No comments:

Post a Comment