My Hubby Henry Kilewo.
Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote.
Nimeolewa
na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa
Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa (nahudumia watu wote wenye vyama na
wasio na vyama).
Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"
Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu
fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake
aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli
HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi
yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa
ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.
Hubby Henry Kilewo kikazi zaidi.
Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA
MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano
Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu
yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????
My family, Hubby Henry With Our Boys, Lincon na Linston.
Fans Wangu wote naamini mtakuwa
mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu,
Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA
ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE.
No comments:
Post a Comment