Pages

Translate

Thursday, 25 July 2013

BINTI ALIYEZALIWA BILA MACHO WALA PUA ATAKIWA KUTOA UBAVU WAKE ILI AFANYIWE UPASUAJI


Msichana Brave Cassidy Hooper (17) kutoka Charlotte, Kaskazini mwa Carolina Marekani aliyezaliwa bila pua wala macho anategemea kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kurekebisha uso wake.
u-4
Brave anategemewa kufanyiwa upasuaji huo (July 31) mwaka huu ambapo inategemewa sehemu ya mfupa utaondolewa katika ubavu wake kwaajili ya kutumika kutengeneza paji la uso wake, mfupa huo utasaidia kama kiunganishi cha pua mpya atakayowekewa.
 
Msichana huyo ambaye yuko excited kwa ajili ya upasuaji huo mkubwa, tayari ameshafanyiwa upasuaji mara kadhaa kama sehemu ya maamdalizi ya upasuaji huo.
u-5
Imechukua miaka sita kwa madaktari kufanya mchakato wa kutengeneza misingi ya kufika hatua ya kuwa katika nafasi ya kutengeneza pua mpya kwa Cassidy.
 
Katika siku za nyuma, Cassidy alikuwa akitumia macho ya bandia, lakini kutokana na wazazi wake kushindwa kumudu gharama kubwa za $ 5,000 kila moja hakuendelea kuyatumia, kutokana na mahitaji ya kuyabadilisha kadri Hooper alivyokuwa anazidi kukua.
u-3
Hooper amesema yuko excited kwaajili ya upasuaji huo mkubwa ambao anaamini kama utafanikiwa utamfanya aweze kupata pua na kunusa kama binadamu wengine.
Mtazamae hapa

No comments:

Post a Comment