Pages

Translate

Tuesday, 23 July 2013

BABA AUA MTOTO WAKE WA MIAKA MIWILI KWA KOSA LA KUTAPIKA...


 
Mtoto wa miaka miwili amefariki baada ya baba yake kudaiwa kumtupa kitandani - na kusababisha mtoto huyo wa kiume kujibamiza kichwa chake ukutani - kwa sababu alitapika.
Mama wa Jayden Morales Villegas 
alikubaliana na uamuzi wa kumtoa mtoto huyo kwenye mashine kuokoa maisha Jumapili mchana, siku tano baada ya kudaiwa kupasuka akiwa mikononi mwa baba yake, Angel Villegas, mwenye umri wa miaka 29.
Shambulio hilo linadaiwa kutokea wiki mbili tu baada ya Jayden na kaka zake watatu kutolewa kwenye mikono ya uangalizi wa mama yao na Idara ya Watoto na Familia na kuhamishiwa kwa baba yao.

Villegas, baba wa watoto tisa, alikuwa akimtunza mtoto huyo na baadhi ya ndugu zake kwenye makazi yake huko Homstead, Florida Jumanne ndipo mtoto huyo, ambaye alikuwa akisumbuliwa na baridi, alitapika wakati wa chakula cha usiku.

Alichanganywa na mtoto wake na kumtupa kitandani, kumsababishia mtoto huyo kugonga kichwa chake ukutani. polisi walisema. Alimkuta mtoto huyo akiwa hajitambui siku iliyofuata, kiapo chake kilisema.

Mtoto huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Watoto ya Miami, ambako alitangazwa ubongo haufanyi kazi na kuwekwa kwenye mashine ya kuokoa maisha. Lakini alitangazwa kufariki Jumapili Saa 7:30 mchana.

"Inauma mno, alikuwa tu mwanangu," mama wa Jayden, Vanessa Morales alieleza. "Nilimweleza tu awe jasiri, kwamba tunampenda na kaka zake wanampenda na kwamba kamwe sitaweza kumsahau."

Villegas alikamatwa na mashitaka yake yameongezwa kutoka kujaribu kuua hadi kuua na kudhalilisha mtoto kwa kiwango cha juu.

Morales aliongeza kwamba alishitushwa na kukamatwa huko.

"Chizi, anayechukiwa na aliyechanganyikiwa kabisa sababu sikufikiria kabisa angeweza kufanya kitu kama hicho," alisema. "Kwanini hakuelekeza hasira zake kwingineko mbali na mtoto huyo wa miaka miwili, hususani mtoto wake, mtoto wake."

Ukurasa wake wa Facebook ulitawaliwa na picha zake na watoto wake, wakiwamo watoto wawili wa kiume na mtoto wa kike.

Watoto wote wa Villegas na wa Morales wamebaki chini ya uangalizi wa Idara hiyo ya Watoto na Familia.

Villegas anashikiliwa kwa dhamana ya Dola za Marekani 110,000 lakini kama akilipa kiasi hicho, atawekwa chini ya ulinzi nyumbani

No comments:

Post a Comment