WATUMISHI
wa Shirika la Umeme Nchini( Tanesco) wameaswa kufanya kazi zinazohusu Shirika
hilo pekee na siyo kujihusisha na kazi za Ukandarasi, hali inayosababisha
mgongano wa Maslahi kato yao na Wakandarasi.
Aidha
imeelezwa kuwa Mtumishi atakayebainika kujishughulisha na kazi ambazo zinatakiwa
kufanywa na Mkandarasi ajitoe kabisa katika Shirila ka Tanesco ili aendelee na
kazi hiyo ambapo pia Wakandarasi wanajiingiza katika Shughuli za Tanesco pia
wameatakiwa kuacha.
Agizo
hilo lilitolewa na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya Injinia Amos Maganga katika
Mkutano wa Uongozi wa Tanesco Mkoa wa Mbeya na Wamiliki wa Makampuni ya
Ukandarasi wa Umeme na wanachama wa Chama cha Wakandarasi wazawa Tanzania wa
Mkoa wa Mbeya (TLCO) uliofanyika katika ukumbi wa Mkapa Jijini
Mbeya.
Aidha
katika Mkutano huo ambao awali Raisi wa Chama cha Wakandarasi Wazawa Tanzania
(TLCO) Kura Mayuma, alisema Tanesco na Wakandarasi ni wadau muhimu wa kumsaidia
Mwananchi lakini wanashindwa kufikia mwafaka kutokana na kuwepo kwa
Changamoto.
Alizitaja
changamoto hizo kuwa ni pamoja na kutokuwa na Mahusiano mazuri kati ya
Wakandarasi na Watumishi wa Tanesco, Watumishi wa Tanesco kufanya kazi za Umeme
sambamba na wakandarasi ambapo alisema Chama kimepata malalamiko kuwepo kwa
watumishi ambao huchukua na kufanya kazi za kikandarasi.
Alisema
kutokana na kuingiliana huko kunawafanya Wakandarasi kuishi maisha ya kuviziana
kwa kuwa wateja wengi hasa vijijini humwamini zaidi Mtumishi wa Shirika kuliko
Mkandarasi ambaye ndiye mwenye jukumu la kutengeneza
umeme.
Changamoto
zingine ni Vifaa vya kufanyia kazi kutotosheleza, Mamlaka zingine za Kiserikali
kama Tamesa, Nhc, Wakala wa majengo, Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji
kufanya kazi za Wakandarasi, upimaji wa Service line kuwa na kasoro, Vishoka,
kutotambuliwa kwa Wakandarasi na ofisi ya Tanesco.
Zingine
kutokupewa kazi za kusambaza umeme (kujenga service line), upendeleo wa ajira,
kitengo cha umeme wa dharula kuchelewa kufika eneo la tukio na Malalamiko ya
wateja kuwa Shirika haliwamilikishi moja kwa moja wateja mali
wanazolipia.
Kwa
upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya Injinia Amos Maganga, alikijibu
baadhi ya Changamoto hizo alisema Tanesco na Wakandarasi wote kwa pamoja
wanadhana moja ya kuhakikisha mteja wanatendewa haki.
Alisema
ili kurudisha mahusiano mazuri kati ya Watumishi wa Tanesco na Wakandarasi ni
pamoja na kukutana mara kwa mara kwa kufanya mikutano ambapo katika Mkutano huo
iliadhimiwa kukutana kila baada ya miezi 6.
Maganga
aliongeza kuwa Mahusiano pia yatakuwepo endapo Mkandarasi atafanya kazi yake
bila kuingilia majukumu ya Tanesco kama vile Watumishi wa Tanesco kutengeneza
umeme hadi kwenye mita na siyo kuingia ndani ya nyumba ya
mteja.
Pia
alisema Wakandarasi hawaruhusiwi kupanda kwenye nguzo na kugusa mita kwa kuwa
jukumu hilo ni la wataalamu wa Tanesco na kuongeza kuwa iwapo Mkandarasi
atakutwa kwenye nguzo atachukuliwa hatua kama kishoka wa
umeme.
Alisema
baadhi ya Wakandarasi kuhusishwa na wizi wa Umeme ambapo baada ya kukamatwa kwa
wezi huwataja wao, pia kupitisha kazi zisizokuwa na sifa, Mihuri yao kutumika
vibaya na kujengwa laini zisizohalali na kupitishwa na Mkandarasi bila kupitia
taarifa Vizuri.
Aliongeza
kuwa Changamoto nyingine inayofanywa na Makandarasi ni ulanguzi wa Fomu ya
Maombi ya mteja ambazo huziuza kati ya Shilingi 50,000/= na 80,000/= ili hali
bei hali ni Shilingi ni kati ya 6000/= na 10,000/=.
Hata
hivyo kutokana na kukithiri kwa hali hiyo Meneja huyo alisema baadhi ya
Wakandarasi wameacha kazi zao na kujishughulisha na ulanguzi wa Fomu hivyo
kuagiza kuwa Mkandarasi hata husika na kumchukulia fomu
mteja.
“
Kuanzia leo nasema Mteja akiwa na picha yake atanunua fomu ndipo atakapomtafuta
Mkandarasi kwa ajili ya taratibu zingine maana hii tabia imesababisha hata fomu
kuisha mapema kutokana na baadhi yao kuhodhi fomu nyingi na kuzunguka kwenye
makorido ya Ofisi za Tanesco ili kuvizia wateja” alisema Meneja
huyo.
Aidha
aliwahimiza Wakandarasi kuheshimu ofisi zao kwa kutulia na kusubiri wateja na
siyo kuwavizia wateja kwa kuwalangua bei ya Fomu na kumlazimisha kumfanyia
kazi.
Na
Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment