Pages

Translate

Wednesday, 19 June 2013

KIBAO KIMEMGEUKIA MWENYEWE BAADA YA KUKATAA KUMUUA KAMANDA WA TAKUKURU MBEYA, KIJANA ATEKWA NA KUTESWA, ABAMBIKIZWA KESI POLISI. KUFIKISHWA MAHAKAMANI KESHO



KIJANA Ally Mohamed Ally, kesho anatarajia kufikishwa katika mahakama ya mwanzo Mbeya mjini baada ya kubambikizwa kesi ya wizi wa vitabu vya kukusanya ushuru.
Kesi hiyo inakuja siku chache baada ya kijana huyo kutumwa kufanya mauaji ya viongozi wa TAKUKURU mkoani Mbeya akiwemo Kamanda wa Takukuru mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka, ambapo kijana huyo hakuweza kutimiza matakwa ya maboss wake waliomtuma.
Akizungumza na blog ya kalulunga.com huku akivua nguo na kuonesha michirizi ya kucharazwa viboko akiwa uchi baada ya kutekwa, kijana huyo alisema kuwa, jana eneo la Calnival mafiati Mbeya alitekwa na kuingizwa kwenye ofisi moja ya kukusanya ushuru na kuvuliwa nguo kisha kuanza kucharazwa viboko kama adhabu ya kutotekeleza mauaji yaliyopangwa kwa viongozi wa serikali.

Kijana huyo mwenyeji wa Unguja Zanzibar, huku akibubujikwa na machozi alisema aliokolewa na polisi lakini alipofika polisi alipewa kesi ya wizi wa vitabu jambo ambalo amesema anamuachia Mungu na kwamba kisa ya hayo yote ni visa na sasa amepata kazi katika kampuni nyingine ambayo imepata tenda hiyo ya kukusanya ushuru, hali iayomuhatarishia maisha yake kutoka kwa maboss wake wa awali.
Amesema Maboss wake wa awali wameahidi kumfunga gerezani kwa kumbambikiza kesi au kumuua kwa njia yeyote ile kwa gharama yeyote.

 Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka aliyekusudiwa kuuawa.

No comments:

Post a Comment