NA DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja jana usiku alinusurika kifo baada ya kugonga nyumba wakati akijifunza kuendesha gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 952 BTJ.
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja jana usiku alinusurika kifo baada ya kugonga nyumba wakati akijifunza kuendesha gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 952 BTJ.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku maeneo ya uwanja wa ndege jirani na Chuo cha Ujenzi njia panda ya kuelekea gereji ya Msuya.
Mbali na mwanamke huyo kunusurika kifo, pia familia iliyokuwa ikiishi kwenye nyumba iliyogongwa nayo ilinusurika baada ya gari hilo kuvunja ukuta wa nyumba na kuingia mpaka chumbani ambako familia ilikuwa inajianda kulala.
Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mtandao huu walidai kwamba mwanamke huyo ambaye bado hajaiva kwenye udereva alikata kona iliyo eneo hilo kwa mwendo kasi.
Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mtandao huu walidai kwamba mwanamke huyo ambaye bado hajaiva kwenye udereva alikata kona iliyo eneo hilo kwa mwendo kasi.
"Huyu mama anajifunza kama unavyoona kibao cha 'L' kwenye gari yake, uzembe alioufanya alikata kona hii kwa mwendo wa kasi na kwamba badala ya kukanyaga breki alikanyaga moto na kuzidisha kasi ndipo alipogonga nyumba hii." Alisema shuhuda mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jumanne Athuman.
No comments:
Post a Comment