Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua
mkutano kati ya waandishi wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo
Kisanji(TEKU)
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
wakifuatilia kwa umakini kikao hicho wakati kikiendelea
Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye pamoja na
katibu wake wakisikiliza kwa umakini wahadhiri wakichangia hoja
Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo
Kisanji(TEKU) , akikazia jambo ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa
Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo
Kisanji(TEKU), akitila mkazo na kujibu swali ambalo liliulizwa na mmoja wa
waandishi wa Habari.
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
wakipiga piga Meza kuashiria kuunga MKONO Hoja ilizo somwa.
Kikao kikiwa kinafungwa kwa Sala
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)
wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa
anauficha Uso akihofia kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari
kuhusiana na Mgogoro unao endelea Chuoni hapo
HALI si Shwari Ndani
ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili
wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani
ya kufungia Mhula, Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu
kwa kile walichodai Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo
yao.
Mgomo huo umetangazwa
leo na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho kilichopo Block T kata ya Iyela
Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili
30.
Simbeye amesema kuna
mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya
Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini
hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa
ushirikishwaji wa maamuzi yanayohusu Taaluma.
Kwa taarifa zaidi na
madai ya Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza
muhula inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye barua hapo
chini lakini habari kamili itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa
nasi.
PICHA , HABARI NA MBEYA YETU
No comments:
Post a Comment