Mtambo wa Wachina ukinyenyua gari la Kampuni ya Sabena baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi. |
Wachina
wanaojenga barabara ya Chunya wakishangaa gari la Kampuni ya Sabena
baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya Chunya
likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.
Majeruhi wa ajali hiyo Ramadhani Kipese (45) akiwa na majeraha kichwani. |
Kondakta
wa gari la Kampuni ya Sabena Seif Salum (34) akisaidia kuokoa mizigo ya
abiria baada ya kupata ajali eneo la maji mazuri Kawetere barabara ya
Chunya likiwa linaelekea Tabora leo Asubuhi.
Gari la Polisi likiwa eneo la tukio kuokoa mizigo ya majeruhi walolazwa katika Hospital ya Rufaa ya Mbeya.
********************************************
KICHANGA cha Miezi 6 kimefariki dinia papo hapo na wengine zaidi ya 60 wamenusurika kufa katika ajali mbaya iliyohusisha Basi kampuni ya Sabena baada ya kuacha njia na kutumbukia katika Mtaro pembezoni mwa Barabara eneo la Maji mazuri Kawetere nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
Kwa
mujibu wa Wahanga wa ajali hiyo iliyotokea jana wamesema imetokana na
mwendokasi ambapo Dereva alishindwa kulimudu basi hilo lililokuwa
likitokea Mbeya kuelekea Mwanza.
Wamesema ajali hiyo imetokea majira ya Saa moja asubuhi ambapo
katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa na kukimbizwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mbeya huku wengine wakipatiwa huduma ya kwanza
kisha kuendelea na safari baada ya kubadilishiwa gari.
Gari
hilo lenye namba za usajili T 887 AYG liliharibika vibaya na kushindwa
kuendelea na safari ndipo lilipoletwa basi lingine kampuni hiyo hiyo ya
Sabena kwa ajili ya kuendelea na Safari.
Kondakta
wa Basi hilo Seif Salum(34) amesema chanzo cha ajali hiyo ni ubovu wa
gari uliosababisha kupasuka kwa mpira wa Breki hivyo gari kushindwa
kusimama na kutumbukia mtaroni.
Amemtaja
Dereva wa basi hilo kuwa ni Suddy Hussein ambaye inasadikika kuwa
alikimbia baada ya ajali hiyo ingawa kondakta alitoa taarifa kuwa
kafuata matibabu Hospitalini.
Picha na Mbeya yetu.
No comments:
Post a Comment