Pages

Translate

Sunday, 2 February 2014

KWA SUPOTI YAKO NDOTO YA TAJI LA MISS WORLD KUJA TANZANIA YAWEZEKANA


Hey guys. At Miss World, contestants usually need as much support as they  can get. I would therefore like to ask for your help in spreading the  word to your fellow fans, friends, family, acquaintances etc. about the  representative for Tanzania this year; Happiness Watimanywa.

People around the world can help me make an even bigger impact through social media and I would like you to be informed of my journey from as early as now.

Please follow: @misstanzania2013 on Instagram
@misstz2013 on twitter   And Like Miss World-Tanzania on Facebook
Thanks for the support. Happy

HILI NDILO GARI LILILOUA ASKALI WA 5 DODOMA JANA



Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Askari polisi watano mkoani dodoma wafariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya 23.45 hrs katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa Polisi Wilaya ya Kongwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano papohapo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1.          D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2.          F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3.          H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4.          WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5.          WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe. 
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.

Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea. Miili ya maerehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.

Aidha Kamanda MISIME ametoawito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

KANISA LAUZA SAKRAMENTI SH 10,000, WAUMINI WALALAMIKA

WAUMINI wa Kanisa la Break Through Assemblies lililoko eneo la Boko Magengeni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam linadaiwa kuuza Sakramenti kwa Sh 100,000 kwa kila muumini.
Hatua hiyo inadaiwa kuwanyima wasio na fedha chakula hicho cha Bwana hivyo kusababisha malalamiko dhidi ya uongozi wa Kanisa hilo la Walokole.

Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili, zilisema tukio hilo lililoshangaza waumini lilitokea Januari 19. Kanisa hilo linaongozwa na Mchungaji Godfrey Simtomvu.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, na kwa masharti ya kutotajwa majina, waumini walisema kitendo hicho kiliwashangaza siku hiyo kanisani hapo walikokuwa wamekwenda kwa ajili ya Ibada kama siku zingine.

Akisimulia, mmoja wao alisema baada ya Mchungaji kuhubiri, vililetwa vikombe na mikate ambayo hutumiwa kanisani kama ishara ya kushiriki pamoja Chakula cha Bwana. Makanisa mengine hutambua ibada hiyo kama ya Sakramenti ya Chakula cha Bwana.

“Baada ya vifaa hivyo kufika kanisani hapo vilionekana kuwa vichache tofauti na waumini waliokuwa kanisani hapo…ndipo Mchungaji alipopaza sauti kuwa mwenye Sh 100,000 na zaidi ndiye atakayeshiriki,” alisema na kuongeza kuwa Januari 26, alishindwa kuabudu kutokana na kitendo hicho.

Alisema baada ya kutamka hivyo, waumini wengi walinywea wakashindwa kusogea na kupisha watu wapatao 10; lakini baada ya kuona idadi imekuwa ndogo zaidi ikatangazwa kuwa hata wenye Sh 50,000 wanaweza kusogea mbele kushiriki.

Aliongeza kuwa wakati wote huo waumini walikuwa wakitazamana, wakijiuliza juu ya utaratibu huo mpya, jambo ambalo ni kinyume na ilivyokuwa awali kanisani.

Alisema Mchungaji baada ya kuona idadi ya waumini inazidi kupungua, akawatangazia kuwa wasiokuwa na fedha wajiandikishe kisha wapokee chakula hicho kisha na kesho yake wapeleke kiwango hicho cha fedha. Muumini mwingine alisema jambo lililoshangaza wengi ni utaratibu huo mpya ambao awali haukuwapo kwani walikuwa wakitangaziwa wiki moja kabla na kutakiwa kujitayarisha kwa ajili ya ibada hiyo ya Chakula cha Bwana.

“Awali Mchungaji alikuwa akitupa taarifa wiki moja kabla, akiwataka waumini kujitayarisha na kusafisha nyoyo zao kabla ya kushiriki kitendo hicho ambacho tuliamini kuwa ni kitakatifu na chenye mafundisho makubwa kwa waumini,” alisema na kuongeza kuwa hilo la kununua chakula lilizuka ghafla na hakujua hatma yake.

Mwingine alisema mbali na kununua chakula hicho, pia jambo lililozusha mshangao kwa waumini ni Mchungaji huyo kuleta watu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuhubiri Neno la Mungu akidai kuwa ni wahubiri ambao nao husisitiza neno la kutoa tu.

“Waumini tunaamini kuwa Bwana Yesu alitoa chakula hicho bure…iweje leo waumini wauziwe tena kwa kupangiwa kiwango?” Alihoji.

Akizungumzia madai hayo, Mzee wa Kanisa hilo alisisitiza kuwa yeye si msemaji wa Kanisa hilo na kusema madai hayo hayana ukweli na kwamba siku hiyo, Mchungaji hakumaanisha kwamba utakuwa utaratibu, bali ilikuwa ni kuhamasisha utoaji kwa muumini mwenye nacho. Alisema kufanya hivyo halikuwa lengo la kutafuta fedha bali kupeleka Neno la Mungu mbele.

“Msemaji wa Kanisa ni Mchungaji mwenyewe, ukiniuliza sana mimi utakuwa unanionea, kama unamtafuta na ukamkosa atakuwa redioni katika kipindi,” alisema mzee huyo.

Akizungumzia malalamiko hayo, Mchungaji Simtomvu alisema kutokea kwa hali hiyo si imani ya Kanisa hilo bali ilitokana na mhubiri kutoka Kongo ambaye alifunuliwa na Mungu na kutaka waumini kuweka maagano yao na Mungu kwa mwaka huu.

Alisema hayo yalikuwa mafunuo ya mtu na si imani na ni kitu ambacho hutokea mara moja tu na kutolea mfano wa yai linapouzwa kwenye mnada kwa bei kubwa, ingawa bei yake halisi inajulikana.

“Laiti ningemfahamu aliyeleta taarifa hiyo ningemsaidia, kwani amekengeuka, mbona Mchungaji TB Joshua wa Nigeria huuza maji katika vichupa vidogo kwa gharama kubwa inayoweza kufikia Sh 75,000,” alisema Mchungaji Simtomvu.

Alisema tukio hilo ilikuwa ni kwa muumini anayetaka kuweka agano na Mungu wake, kwamba mwaka huu amtendee mambo gani na kuhoji kuwa zipo imani za ajabu ajabu lakini haziripotiwi.HABARILEO

Saturday, 1 February 2014

KIKONGWE AFUMWA CHUMBANI KWA MTU AKIWA UCHI

Mashuhuda wa mwanzo wanadai walimkuta bibi huyo akitapatapa bila kujua nini la kufanya huku akiwa mtupu na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kilichotafsiriwa kwamba pengine bibi huyo anaweza kuwa mchawi,huku wengine wakisubiri taarifa ya polisi na wengine wakisema huenda bibi huyo alipatwa na matamanio ya kimwili.
Hili ni tukio lilitokea huko Bukoba ambalo linamhusisha Kikongwe mmoja ambaye jina lake bado halijapatikana kukutwa chumbani kwa mtu huku akiwa mtupu chumbani kwa mtu.
25Mpaka sasa bado haijajulikana kama ni Kigarura au pengine alipata matamani ya mwili akaona pengine chumba kile kingemfaa kumpatia msaada wa mambo yake.
28Bibi Kizee huyo anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 70,ambapo amekamatwa alfajiri ya leo January 31 hata hivyo polisi wamefanikiwa kumnusuru na kifo baada ya kumchukua na kumpeleka kituo cha polisi.
30Mashuhuda wa mwanzo wanadai walimkuta bibi huyo akitapatapa bila kujua nini la kufanya huku akiwa mtupu na nguo zake zikiwa pembeni kitendo kilichotafsiriwa kwamba pengine bibi huyo anaweza kuwa mchawi,huku wengine wakisubiri taarifa ya polisi na wengine wakisema huenda bibi huyo alipatwa na matamanio ya kimwili.

UJUE UTAJIRI WA LOWASA

  Tokea enzi ya uhai wa Julius Kambarage Nyerere Faili la LOWASA kufahamika kuwa na utajiri wa kutosha linafahamika sana,na haijaanza leo kwa Lowasa kusemwa na kupewa shutuma kama hizo wala hazikuanza jana.

Zimeanza tokea kipindi Mwalimu Nyerere yuko hai,na hadi alishafikia hatua ya kuhoji utajiri wa Lowasa enz hizo akiwa kijana kama wa miaka 42 hivi,na kwa wakati huo miaka 42 huonekana kijana kweli kweli tofauti na sasa vijana katika umri kama huo washakuwa wazee tayari kutokana na ugumu wa maisha na frustuations zake.

Je,unafaham ni kwa nin MALECELA kwa kawaida tuh tokea hapo kale hampendi Edward Lowasa??

Hii vita haikuanza leo.,wanaccm hawa wawili na wenye ushawish kwenye chama hiko wameanza msuguano na malumbano tokea enzi hizo John Malecela akiwa Waziri Mkuu na Lowasa akiwa Waziri mwandamizi katika ofisi ya waziri ya waziri mkuu,kwa mantiki hiyo kwamba alikuwa chini ya malecela na kwa kumsaidia majukumu ya kazi ya siku zote za kuendesha serikali.

Enzi hizo wabunge wa jamhuri ya muungano wa tanzania walikuwa hawana magari ya kusafiria kama haya wanayokopeshwa kwa sasa,hali iliyokawa inawapa ugumu sana kuwatembelea wananchi wao majimboni hata wakati mwingine ugumu pia wa kuwahi bungeni kwa wakati kutokana na aina ya magari waliyokawa wanayatumia kipindi hiki kukosa stability ya kumudu safari na ukizingatia ubovu wa bara bara wa kipindi huko maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.

Hili suala lilikua linaumiza sana serikali kipindi hiko chiniya utawala na usimamiz wake wazir mkuu wa kipindi hicho ndug john malecela.

Kutokana na kuwaza na kuwazua likaja wazo la kupeleka idea kwa serikali ya watu wa japan ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kuwasaidia kihali na mali ili iweze kujikwamua katika tatizo hilo,

Mungu si Athumani,serikali ya japan enzi hizo wakakubali kuwaunganisha serikali ya tanzania na kiwanda cha toyota na kuwapa ushirikiano wa hali ya juu katika mazungumzo baina yao na kiwanda hicho hadi ikafikia tamati ya makubaliano kwamba serikali ya tanzania inaweza kukopeshwa magari hayo kisha wakawa wanalipa pole pole ili kusaidia kukizi na kuikubali changamoto hiyo.

Serikali baada ya kufanikisha plan hiyo ikaja kwa wabunge na kuwaeleza kwamba wanaweza kukopeshwa magari kwa mkopo,wabunge waliingia na wasi was kias flan na kusema wao wataweza kulipa vpi gharama hzo ukizingatia pesa waliyokawa wanachukua kipindi hiko isingetosha kulipa mkpo huo??

Serikali kupitia kw wazir mkuu malecele wakawaambia nyinyi chukuen tuh,sisi serikali tutajua tunawasaidia vipi,kwaiyo chukuen kwanza ili mukabiliane na changamoto ya usafiri kwanza.

Wabunge walikubali wazo lile na deal likafanyika,mambo yakafana kisawa sawa.

Sasa baada ya hapo mtu pekee ambae alikuwa anafuatilia mchakato mzima ni wazir wa nchi ofisi ya wazir mkuu enzi hizo akiwa ni edward lowasa,alikuwa anafuatilia suala hilo kwa ukaribu sana.


Wale wajapan walipolipwa chao,kumbe kuna makubaliano ambayo yakishafiikiwa baina yao na wazir mkuu malecela ya kumpatia kifuta jasho kwa kufanikisha deal ile kufanyika kwa ukamilifu wake.

Na yasemekana kifuta jasho hiko kilikuwa cha maana sana,cha maana sana sana,

Bahati mbaya sana wale wajapan walipofika ofcn kuleta kifuta jasho kile walianzia kwanza kwa ofisi ya wazir wa nchi ili wapate nafas ya kumuona wazir mkuu,sasa walipokutana na lowasa yasemekana akawauliza mnafuatia nin tena mheshimiwa ili hali deal ilishafanyika kikamilifu??kwan kuna tatizo??wale wajapan wakamwambia kwamba kuna kifuta jasho yapasa tumkabidh muheshimiwa wazir mkuu malecela.

Lowasa,,akastaajabu..!!akasema ,,"mnasema"???hicho kifuta jasho mnataka kumfikishia vipi mheshimiwa hamjui kuwa yule ni mtu mkubwa sana??kuna utaratibu wa kumfikishia kwa protokali ya serikali,sasa sikilizen bwana....

Hiyo pesa nipen mimi nitamfikishia,kwan kwa sasa hata hivyo yupo safarin hadi arudi,so nipeni mimi nitamkabidh,wale wajapan kwa kuwa wanafaham katika mchakato mzima wa ile deal lowasa nae alikuwa anaifuatilia kwa karibu hawakuwa na was was sana kumwachia amana kama ile.,,wakamwachia na kusign nae kisha wakageuza zao.

Kilichotokea hapo sasa mungu mwenyew ndie anaejua,

Lowasa akapiga kimya,kimya na yeye,yeye na kimyaa,muda ukawa unazid kwenda naskia ile pesa akaanza kuifanyia michakato ya kuizungusha na kuwekeza kwenye biashara ya real estate kwa haraka haraka na kuzikodisha kwa taasisi binafsi hata balozi mbali mbali za nchi mbali mbali,

Naskia ipo moja ambayo aliikodisha kwa ubaloz wa south afrika hapa hapa nchini,na hadi leo naskia iyo nyumba ni mali ya lowasa pamoja na vitu vingine vingi,kwa ufupi lowasa kawa DON tokea kitambo sana.

Sasa maskin mzee malecela akaona siku zinakwenda na kifuta jasho kutoka japan hakifiki,,akaamua kunyanyua simu na kuwavutia uzi jamaa na kuwauliza,ebwan vipi ile kitu yangu??mbona nyinyi wajapan wabaya kias hiko??ina maana baada ya deal kufanyika mnatupa jongoo na mti wake??

Wajapan wakasema Booossi,mbona kifuta jasho tulishaleta mda mrefu sana??tulimkabidh bwana Edward yule wazir wako wa nchi katka ofc yako na alisema atakukabidh kwan ulikuwa safarini..!!!

Malecela kikamshuka,kikampoa na asijue hata awajibu nini,

Ikabid sasa amwite edward na kumuuliza,wewe edward pesa yangu iko wapi??na nani alikuambia uichukue kwa niaba yangu??

Edward akasema Boooss,kwa kweli pesa nilichukua lakin sasa kwa kuwa ulikua safarini nikaona niiweke kwanza hadi urudi,,sasa kama unavyojua pesa tena mzee,kulitokea fursa za uwekezaji nikaamua kujikopesha ili niizungushe kisha nitakurejeshea lakin sasa mambo hayajaenda kama yalivyopangwa ndio kwa maana unaona kimya hiv sijakutafuta.

Sasa malecela presha ikampanda na kumshukaaa,atasema nini??na ile pesa ni chafu na ya deal ukizingatia yeye ni wazir mkuu??kumbuka nyerere yupo hai kipindi hicho na akifaham ishu kama hizo panakua hapatoshi..!!

Ikabid malecela ajikaze kisabun na kufa na tai yake shingoni huku lowasa akiendelea kupimp na kujitanua kwa raha zake.

Kwa kias kikubwa hapo ndipo LOWASA alipoanza kuwapiga GAPE LA KIPATO wenzake walio wengi,na kwa kias kikubwa wenyewe hao ambao wako ndan ya system wanalijua hilo.

Ndio kwa maana tokea zama hizo VITA baina ya LOWASA na MALECELA haiwez kuisha kamwe,kwan mambo waliyofanyiana wawili hao yanatishaa.

Hiyo ndiyo siasa ya bongo ilivyo,DO OR DIE.

CLAB YA WAKRISTO YAFUNGULIWA DAR, WATU WAHOFIA MAADILI YA KIKRISTO KUVUNJIKA


Klabu ya nyimbo za injili iliyofunguliwa jijini Dar es Salaam  

Mchungaji Harris Kapiga wa kanisa la Nchi ya Ahadi lililoko Sinza Kamanyola, ameamua kuanzisha klabu ya usiku kama zilivyo klabu nyingine za starehe.
Klabu hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni maeneo ya Mbezi Tangibovu katika hoteli inayoitwa Mak Hotel, imeonekana kuvutia vijana wengi ambao walionekana wakifurahia mandhari na muziki uliokuwa ukipigwa ndani yake.


Tofauti na klabu nyinginezo, Mchungaji Kapiga anasema kutakuwa na udhibiti wa vishawishi vya dhambi ikiwa pamoja na ulevi, mavazi yasiyo na staha na aina ya muziki unaopigwa.
Anasema tangu alipoanzisha wazo hilo, watu wengi hasa wachungaji walikuwa na wasiwasi kuhusu vishawishi hivyo.
“Tangu nimeanza wazo langu hili nimekumbana na vikwazo vingi. Imeshtua watu wengi, japo wengi wamelikubali na kuna baadhi hawakubali ila hawawezi kusema wazi,” anasema na kuongeza:
“Wengine wanajiuliza nitawezaje kudhibiti vipi hali ya klabu kwa sababu maeneo haya kunakuwa na anasa, ulevi na masuala ya mavazi watu watavaaje, na mimi nawajibu.”
“Mtu akija hapa na mavazi mabaya hataingia, tutakuwa makini sana katika hili. Mtu avae nguo yenye staha, siyo mtu aje nusu uchi, tutamtoa kwa nia njema tu. Hata mtu aliyelewa tutamtoa labda tusimgundue.”
 
Mchungaji Kapiga anasema alianza kupata wazo hilo siku alipokuwa kwenye sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Clouds Media ambako pia ameajiriwa kama mtangazaji baada ya yeye kuitwa mbele kwa ajili ya utambulisho ndipo alipojongea mbele huku akiimba wimbo wa kumtukuza Mungu ndipo ukumbi wote uliposhangilia na kumsapoti kuimba wimbo huo na ndipo alipogundua ya kuwa wapo wakristo wapendao kutoka nyakati za usiku lakini wanakosa sehemu za kwenda.

Hata hivyo baadhi ya wakristo mitaani wanalalamika wakidai kuwa ukristo unapoteza muelekeo kwa kufanya mambo kama kwenda club. Lakini pia wapo wengine waliofananisha club hiyo na mikesha inayofanyika katika nyumba nyingi za ibada karibu kila ijumaa.

MBUNGE ALIYEOLEWA NA KIJANA AACHWA

www.newsaba24.blogspot.comMichael Christian (28) ambaye mwaka jana aliitikisa medani ya siasa Bongo kufuatia kufunga ndoa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila (60) ameibuka na kuanika siri zilizomfanya aamue kuivunja ndoa hiyo na mheshimiwa huyo.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa, Rose-Sweeter Kasikila.

Akizungumza  jijini Dar, Michael alibainisha mambo hayo huku akisema anajuta kwa tukio lile ambalo bado halijamtoka kichwani hadi sasa.


Kijana Michael aliianika siri kwamba ni kuchekwa na marafiki zake wa Bagamoyo mara baada ya kugundua amefunga ndoa na mbunge huyo ‘mzee’.
“Marafiki zangu walianza kunicheka, walisema nimefunga ndoa na mbunge mzee, mama mtu mzima. Nikaanza kujisikia vibaya jambo ambalo sikulipenda hata kidogo,” alisema kijana huyo ambaye ni yatima.
Pia kutokuwepo kwa tangazo la ndoa la siku 21 kama sheria ya nchi inavyotaka ilikuwa ni sababu nyingine ya yeye kumuacha mama huyo. Kuna kifungu cha sheria kinachotaka wachumba wanapotaka kufunga ndoa kutolewa tangazo la siku 21 kwenye mamlaka za kufungisha ndoa hiyo ili kama mmoja wa wahusika ana ndoa inayoishi (halali) aweze kuwekewa pingamizi la kufungishwa ndoa.
Hata hivyo siku ya ndoa yetu hakukuwepo na mashahidi wa pande zote mbili (matroni na patroni) walioandaliwa zaidi ya kuitwa papohapo.
Alimtaja kwa jina moja Mchungaji Mtetumo wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God ‘Mlima wa Moto’ kuwa ndiye aliyesimamia kufungwa kwa ndoa hiyo, Septemba Mosi, 2011 ndani ya ofisi huku milango ikiwa imefungwa.
Alisema pia kwamba, suala la ndoa aliligundua siku hiyohiyo baada ya kufika kwenye kanisa hilo ambapo maandalizi mengine yote yalishafanyika akiwa hajui.
kisha akagundwa yeye ua kuwa katika ndoa yake huwenda hata bahatika kupata watoto na mama huyo kwaku mama huyo tayari anao watoto wakubwa zaidi yake na hata nilipomwambia tuzae alikataa
kitu kingine ni kwamba Alianza kunibana sana, kila hatua ya miguu yangu alitaka kujua inakwenda mpaka wapi! Hii hali nikaiona inanipiga pingu, nikagundua kuwa kumbe mimi sijaoa, bali nimeolewa. Yule mama alinioa mimi, si kwamba mimi nilimuoa yeye, nikasema ili niwe na amani ya moyo ni lazima

“Jambo jingine ambalo pia lilichangia kuamua kuivunja ndoa ile ni baada ya kukumbuka historia ya kukutana kwetu.
“Wakati nipo Hospitali ya Bagamoyo na yeye akiwa pale kama muuguzi mkuu, tulizoeana. Kuna siku aliniita kwake akasema anasafiri anaomba nimwangalizie nyumba, nilikuwa na rafiki yangu tukawa tunalala pale mpaka aliporudi.
“Kuzoeana kuliendelea, mwishowe tukawa wapenzi mpaka ndoa. Nilipokumbuka hivyo tu nikagundua kuwa aliniingiza mapenzini kwa hila au mbinu, hilo pia sikulipenda,” alisema Michael. 

Kijana Michael alisema kutokana na umri wake, ndani ya nyumba alijiona ni mtoto na si mume kama wanaume wengine walivyo.
“Hata uwezo wangu wa mawazo kwake haukuwa wa mume na mke, ni wa mtoto na mama. Kifupi haikuwa ndoa halali,” alisema.
 
Kijana huyo alisema ndoa yake na mheshimiwa huyo aliivunja mbele ya Mchungaji wa Kanisa la Mikocheni ‘B’ Assemblies of God, Dk. Getrude Rwakatare walipokwenda kusuluhishwa ili waende wakaishi kwa amani.
Alisema kabla ya usuluhishi alimfungukia mama Rwakatare kuhusu manyanyaso anayoyapata ndani ya ndoa hiyo ndipo aliposimama na kuivua pete kisha kuitupa chini huku akisema katu hawezi kurudi kwa mkewe huyo na ndoa imevunjika, akaondoka zake.

Kijana Michael alisema kilio chake kikubwa kwa sasa ambacho angependa kifike hadi kwa Rais Jakaya Kikwete ni kitendo cha mkewe huyo kuzuia vyeti vyake ambavyo vingemsaidia kutafutia kazi sehemu mbalimbali.

“Amezuia vyeti vyangu vyote, kila nikimwambia navitaka nikienda ananifanyia visa, nawaomba Watanzania wanisaidie kwa hili.
“Mimi kwa sasa nataka vyeti tu, sitaki cha ndoa wala nini? Lakini hataki kunipa,” alisema Michael.

Akijibu tuhuma hizo, Mheshimiwa Kasikila alikiri kuwa na vyeti vinavyolalamikiwa na mumewe huyo, lakini alikanusha kwa nguvu zote juu ya maneno kuwa yeye ameoana na mtoto mdogo, akirejea vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vinavyomtaja mtoto kama ni mtu wa namna gani.
Mbunge: “Mwandishi, unafahamu mtoto kwa katiba yetu ni mtu wa namna gani?”
Mwandishi: “Ni mwenye umri wa chini ya miaka kumi na nane.”
Mbunge: “Sasa Michael ni mtoto? Ana miaka 28 unamuita mtoto?”

Alisema anajua suala hilo lina shinikizo la kisiasa, kwani hivi karibuni baadhi ya wanasiasa walikwenda jimboni kwake wakiwa na nakala ya gazeti moja lililoandika habari zake na kijana huyo na kuwaambia wapigakura wake kuwa mbunge wao ameoa kitoto, lakini wapigakura wake waliwapuuza kwa kuwaambia hilo haliwahusu kwani wanachojua anawawakilisha vizuri bungeni.
“Kama kweli ninyi mnampenda huyo Michael, muelekezeni sehemu sahihi ya kwenda kupeleka madai yake. Ngoja nikupe mfano, mimi nikiwa wizara ya afya, mtu akija na malalamiko kuhusu pembejeo za kilimo, kwa kumsaidia, nitamuelekeza aende wizara ya kilimo, kwa kuwa pale (afya) siyo sehemu yake, sasa nyinyi muelekezeni huyo sehemu sahihi ya kupata haki yake, siyo huko magazetini,” alisema mama huyo

Kwa upande wake, Mchungaji Rwakatare alipopigiwa simu kwa lengo la kumsikia chochote kuhusu ishu hiyo, alianza kulalamikia habari iliyoandikwa miezi miwili nyuma na kukata simu.