Pages

Translate

Monday, 5 August 2013

HAYA NI MAMBO YANAYOTOKEA BAADA YA ISHU YA MADAWA KUBUMA. TAFADHALI PICHA SI NZURI SANA



Hivi ndio huwa mambo yanavyokuwa kwa wabebaji wa madawa ya kulevya(maarufu kwa jina la Punda)  ni hatari sana kwa afya ya Binadamu, kijana tuungane kwa pamoja kupinga biashara hii haramu na hatari sana tukishirikiana kwa pamoja  na Serikali kwa pamoja tunaweza kutokomeza madawa haya haramu na hatari sana kwa jamii yetu.
Hii ni picha ya x ray inayoonesha ndani ya tumbo madawa aliobeba.
Yanavyoweza kuathili baadhi ya sehemu katika mwili.
Operation ikifanyika tayari kuyaondoa madawa hayo yaliompelekea kijana huyu kufariki.
Operation ikiendelea hatari sana ndugu zangu.
Baada ya utumbo kutolewa tayali kuanza kuyatoa madawa hayo.
Kama uonavyo yakiwa ndani ya utumbo mpana.
Yakianza kutolewa pamoja na kushafishwa jinsi unavyoona katika picha.
Baada ya utumbo kuchanwa tayari kwa kutoa keti hizo.

Friday, 2 August 2013

MKE WA DR. SLAA AZUA TIMBWILI MAHAKAMANI....

 
JOSEPHINE Mushumbusi, mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, jana alisababisha vicheko mahakamani baada ya kushindwa kumtambua mshtakiwa anayedaiwa kumpora maeneo ya SUMA JKT.

Josephine alimuacha mshtakiwam katika kesi yake na kumtambulisha mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.

Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.

Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.

Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.

Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.

Alidai akiwa eneo la tukio katika foleni alimwona mtu akipita mkono wa kushoto huku akimuangalia kwa kutumia kioo cha pembezoni na ghafla alimuona akivunja kioo cha gari lake.

Josephine aliidai alipoanza kuvunja dirisha alitahamaki lakini alisikia risasi hivyo aliamua kutafuta jinsi ya kujiokoa kwa kutoa gari eneo hilo na kwenda katika geti lililopo karibu na Suma JKT.

“Nilifanikiwa kuona sura ya mtu aliyenivamia kwa kuwa tulisimama wote kwa takribani dakika nane,”alidai Josephine.

Josephine alidai katika tukio hilo anakumbuka kulikuwa na watu si chini ya sita na walimwibia vitu mbalimbali. Kesi hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa Agosti 7 mwaka huu

KESI YA WEMA, MAHAKAMA YAFURIKA ATINGA NA WAPAMBE KIBAO WATU WAPAGAWA


KESI ya kudaiwa kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao Meneja wa Hoteli, Goodluck Kuyumbu inayomkabili Staa wa Filamu, Wema Isaac Sepetu imeunguruma Jumatano iliyopita katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar na watu kufurika pomoni, Ijumaa linakumegea kilichojiri.
Katika mahakama hiyo watu walifurika kwa lengo la kutaka kumuona Wema aliyepandishwa mbele ya Hakimu, Bernice Ikanda kusomewa mashtaka ya kudaiwa kufanya vurugu, kushambulia kwa kumpiga makofi na kumtukana Goodluck.

ATINGA NA MSAFARA
Wakati wa kuwasili mahakanai hapo, Wema aliambatana na msafara wa magari matatu, yeye akiwa katika lake la aina ya Audi Q 7, magari mengine yalikuwa ni Toyota Opa na Toyota Hiace yaliyokuwa na watu wake.


WATU WAFURIKA MAHAKAMANI
Kutokana na jamii kupenda kufuatilia matukio ya kila siku ya Wema, watu kibao walifika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo.
Mara baada ya mlimbwende huyo wa mwaka 2006-07 kuzama katika chumba cha mahakama, kulitokea vurugu kwa baadhi ya watu kukanyagana ili kutaka kumuona na kusikilza kesi hiyo kwa ukaribu zaidi.


AINGIZWA CHUMBA CHA MAHAKAMA
Wema aliingizwa katika chumba cha mahakama sambamba na Goodluck ambapo Hakimu Bernice alianza kumuuliza mlalamikaji kama alikuwa na mashahidi walioshuhudia tukio hilo lilivyotokea.
Goodluck alijibu kuwa anao mashahidi na kumwambia hakimu kwamba anaweza kuwaleta mbele ya mahakama hiyo.


KESI YAPIGWA KALENDA TENA
Hakimu aliamuru kesi hiyo iahirishwe hadi Agosti 20, mwaka huu na kumtaka mlalamikaji kufika na mashahidi wake.
Kuonesha kwamba watu wengi walikuwa wamefika kushuhudia kesi hiyo, walitawanyika baada ya uamuzi huo.


WEMA ANUNUA MIHOGO
Mara baada ya kutoka mahakamani na kuruhusiwa kuondoka kutokana na dhamana aliyonayo, Wema alionekana akinunua mihogo kwa ajili ya futari ya siku hiyo.

KANSA YA NGOZI YAMHARIBU MTOTO WA MIAKA 7....BABA AMWAGA MACHOZI AKIOMBA MSAADA



MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani  Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.

Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne.

“Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.

“Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.
TUPE MAONI YAKO KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

Translate

  Imedhaminiwa na Tafsiri
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. MPEKUZI - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger


Chat Full!


MSHILIKI WA SHINDANO LA MISS AFRICA 2010 AUAWA KWA KUCHOMWA VISU

 
 
 Mrembo Linah Keza amekutwa amekufa kwa kuchomwa visu huku binti yake wa miaka mitatu 'akilia pembeni yake kwenye dimbwi la damu'.

Mwili wa Linah Keza, mwenye miaka 29, ambaye inafahamika alishiriki kwenye Shindano la Miss Africa 2010, ulikutwa kwenye ghorofa moja huko King Edward Road, Leyton, juzi mapema asubuhi.

Tukio hilo liliripotiwa kwenye Tume Huru ya Polisi ya Malalamiko, ambayo itatazama mawasiliano yake waliyokuwanayo polisi na mwanaume mwenye miaka 38 ambaye amekamatwa kuhusiana na kifo chake.

Madaktari wa Huduma za Gari la Wagonjwa London waliongozana na polisi kwenda mahali hapo kabla ya Saa 10:30 alfajiri, lakini Linah, raia wa Rwanda anayeishi London, alikuwa ameshatangazwa kufariki eneo la tukio.

Inafahamika kwamba binti yake alikuwa mahali hapo wakati wa shambulio hilo, kwa mujibu wa fafiki mmoja wa familia hiyo.

Herbert Muhire alisema: "Binti (yake) amepelekwa kwenye uangalizi na kupatiwa tiba ya kisaikolojia na matukio mengine baada ya kukutwa akilia kando ya mama yake huyo aliyekuwa amelala kwenye dimbwi la damu.

"Familia na marafiki wameelezewa jinsi alivyokuwa ameuawa na kufa kifo cha kutisha.

Rambirambi kwa Linah kutoka kwa marafiki na jamaa ziliachwa kwenye ukurasa wa Facebook uliofunguliwa mara baada ya kifo chake.

Azun Jezan aliandika: "Huzuni mno, roho yake ilale mahali pema peponi na binti yake na familia wajazwe nguvu katika wakati huu mgumu wa huzuni."

Mwingine, Justine Twongyeirwe, aliandika: "Nitakumbuka tabasamu lako mpenzi Linah. Ulale Mahali Pema."

Jana asubuhi, ukurasa huo ulikuwa na wafuasi zaidi ya 500 na baadhi walituma picha za Linah, ambaye alifanya kazi kama mrembo na kusomea huduma za jamii kwenye Chuo Kikuu cha Wolverhampton.

Kwa mujibu wa polisi, mwanaume huyo mwenye miaka 38 alikamatwa baada ya kujisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi cha north London juzi.

Msemaji wa polisi alisema: "Uchunguzi wa mauaji umeanza baada ya mwanamke huyo kushambuliwa huko Leyton.

"Polisi waliitwa na Huduma za Gari la Wagonjwa London majira ya Saa 10:29 alfajiri ya Jumatano kwa ripoti za kuchomwa kwa visu.

"Maofisa na Huduma za Gari la Wagonjwa walifika na mwanamke huyo mwenye miaka 29 alikuwa ametangazwa kufariki kwenye eneo la tukio."

Uchunguzi wa mwili wake ulipangwa kufanyika majira ya Saa 5 jana asubuhi kwenye Mochari ya Walthamstow.